Klabu ya Simba inajiandaa kuwakabili Ihefu hapo kesho kwenye mchezo wao wa 10 kwenye Ligi ambapo mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

 

Simba Yajiandaa Kuwakabili Ihefu Kesho

Mchezo uliopita Simba ametoka kutoa sare akiwa ugenini, wakati kwa Ihefu wao wametoka kupoteza huku mchezaji wao Juma Nyoso akipata adhabu ya kadi nyekundu ambayo itamuweka nje kwa muda kidogo.

Msimbazi ambao wapo chini ya Juma Mgunda wapo nafasi ya pili kwenye msimamo, baada ya kucheza mechi 9 wakiwa sawa na vinara wa Ligi japokuwa wao wana michezo miwili mbele.

Ihefu bado hali mbaya kwani wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo na katika michezo 9 waliyocheza, wameshinda mchezo mmoja, sare mbili na wamepoteza michezo sita huku matarajio ya kusalia Ligi kuu yakiwa ni hafifu.

Simba Yajiandaa Kuwakabili Ihefu Kesho

Mechi mbili za mwisho kukutana timu hizi mbili vijana wa Mgunda kashinda mechi zote mbili. Na Wekundu wa Msimbazi anataka kulitetea taji msimu huu baada ya kulikosa msimu uliopita kwa watani wenzake Yanga.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa