Klabu ya Yanga imeanza safari ya kurejea jijini Dar-es Saalam baada ya kuondoka na ushindi huko Tunisia dhidi ya Club Africain kwa kuwatandika kwa bao 1-0 ambalo lilikuwa na umuhimu kwao kwani limeifanya liwapeleke hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Yanga Safarini Kurejea Tanzania

Baada ya mechi ya hapa nyumbani kutoa sare ya bila kufungana, mashabiki na wapenzi wa Yanga walianza kukata tamaa kwa kuona timu yao safari ndio imeishia hapo lakini mambo yakaenda vizuri baada ya Kocha wao kumfanyia mabadiliko ya kumuingiza Stephan Aziz Ki.

Aziz Ki ndiye shujaa wa Nasredine Nabi ambaye alienda kubadilisha kila kitu na kufikia dakika ya 79, Wananchi wakawainua mashabiki zao baada ya mchezaji huyo kupachika bao ambalo mpaka dakika ya 90 mpira kumalizika ndilo lililobakia.

Yanga Safarini Kurejea Tanzania

Hivyo kwasasa kilichobakia ni kusubiri hatua ya makundi watapangwa na nani, huku wakiwa bado ni vinara wa Ligi kuu ya Tanzania na baada ya kurejea mechi yao ya kwanza watakipiga dhidi ya Kagera ugenini.

Mara ya mwisho kukutana Yanga dhidi ya Kagera, Young African alishinda mechi hiyo.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa