Ukweli ni kwamba huu siyo wakati mzuri ambao klabu ya Simba unapitia kwani imekutana na matokeo yasiyoridhisha na sasa wameingia kwenye mlundikano wa kuwakosa wachezaji wao muhimu kwa sababu mbalimbali.

Kwenye mechi mbili za ligi walizocheza hivi karibuni Simba wamevuna alama nne pekee, wakifungwa na Azam FC bao 1-0 kwenye uwanja wa Mkapa na juzi wamebanwa mbavu na Singida Big Stars wakiwa ugenini kwa sare ya bao 1-1 na wao wakisawazisha.

Simba, Simba: Peter Banda Nje Wiki Nne, Meridianbet

Sasa mfungaji wa bao la Simba Peter Banda, hakuweza kumaliza mchezo huo baada ya kutoka nje dakika za mwisho akiwa anachechemea na kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally alifungikia ukubwa wa majaraha yake.

Ahmed alisema: “Banda alitoka akiwa anachechemea pale uwanjani. Baada ya vipimo alionekana kuwa amepata shida kwenye enka na kuna uwezekano akaa nje ya uwanja kwa wiki nne.”

“Lakini wakati ikiwa inatazamiwa kuwa anaweza kuwa nje kwa kipindi hicho. Kuna uchunguzi zaidi atafanyiwa na tutawapa ripoti mashabiki wetu juu ya hali hiyo.”

Banda anaongeza idadi ya wachezaji muhimu ambao wanakosekana kwenye timu hiyo kwenye mechi zijazo akiwemo Clatous Chama aliyefungiwa mechi tatu na TFF, Augustine Okrah, Israel Mwenda, Nelson Okwa na Jimson Mwinuke ambao wote ni majeruhi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa