Mchezo wa ligi kuu kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Novemba 27 mwaka huu utapigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Polisi Tanzania kwa msimu huu wametumia viwanja mbalimbali ikiwemo uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na Black Rhino Academy, Karatu baada ya uwanja wao kufungiwa.

Simba, Polisi Kuipeleka Simba Ushirika, Meridianbet

Akizungumzia kurejea kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema: “Mchezo unaofuata tutacheza ugenini dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa ugenini.

“Kikosi kinaendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo, japo hatukuwa na matokeo mazuri kwenye mchezo uliopita lakini bado wachezaji wana morali kwa kuhitaji kuonyesha kile wanachokitamani.

“Tunatarajia kurejea hivi karibuni kwenye Uwanja wetu wa ushirika kutokana na matatizo ambayo tunakutana nayo ya viwanja tunavyotumia kufungiwa.

“Mchezo dhidi ya Simba ambao tutakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani tutaanza kuutumia uwanja wa Ushirika pamoja na michezo mingine iliyobaki ya nyumbani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa