Mchezaji wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya Uingereza James Maddison amefanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Uingereza kilichotangazwa jioni hii kuelekea kombe la dunia nchini Qatar mwezi huu.

Kumekua na minong’ono ya muda mrefu ambayo imekua ikiendelea kutokana na kocha wa timu ya taifa ya Uingereza kutompa nafasi kiungo huyo wa Leicester kwenye timu yake ambayo amekua akiita.maddisonKiungo Maddison amekua akionesha ubora mkubwa kwenye klabu yake ya Leicester kwa misimu kadhaa sasa lakini hakua anaitwa kwenye timu ya taifa ya nchi hiyo chini ya mwalimu Gareth Southgate kitu ambacho kimekua kikiibua mijadala sana juu ya kocha huyo.

Lakini leo hii Maddison ameitwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia mwezi huu nchini Qatar na watu wengi wamepongeza jambo hilo na kueleza kua kiungo huyo amestahili kuwepo kwenye kikosi hicho.maddisonLicha ya wadau kupongeza kuitwa kwa kiungo huyo lakini lawama zimeshushwa kwa kocha Southgate baada ya kuwacha wachezaji kama Fikayo Tomori, Tammy Abraham ambao wameonesha ubora mkubwa kwenye vilabu vyao.

AVIATOR


Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa