Klabu ya soka ya Simba imelazimisha sare ya bao moja kwa moja na klabu ya Singida big stars katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Liti mkoani Singida. simbaKlabu hiyo kutoka mitaa ya kariakoo imebanwa mbavu na klabu ya Singida big stars katika mchezo ambao ulionekana mgumu kwa pande zote mbili, Huku klabu ya Singida ikifanikiwa kupata bao la mapema kupitia kwa Deus Kaseke akimalizia pasi safi ya Said Ndemla.

 

Mechi hiyo ilikwenda mapumziko kwa Singida kuongoza bao moja kwa bila kabla ya kipindi cha pili klabu ya Simba kurudi kwa kasi na kuhitaji kusawazisha bao, Mapema kipindi cha pili Peter Banda aliechukua nafasi ya Mkude akiwasawazishia Vijana wa Juma Mgunda na matokeo kua moja kwa moja.simbaKlabu ya Simba imefanikiwa kufikisha alama 18 huku ikicheza mechi tisa huku watani zao Yanga wakiwa na alama 20 huku wakicheza michezo nane na wakisalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa