Mchezaji wa Kimataifa wa Ufaransa Benjamin Pavard amedokeza kuwa anaweza kuondoka Bayern Munich iwapo atapewa mradi wa kuvutia katika klabu zingine.  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea Bayern mechi 20 msimu huu, akianza mara 16.

 

Pavard Anaweza Kuondoka Bayern Baada ya Kombe la Dunia

Pavard alijiunga na Bayern kutoka kwa wapinzani wa Bundesliga Stuttgart mnamo 2019 na ameshinda mataji matatu ya ligi kuu ya Ujerumani wakati wake na wababe hao wa Bavaria, na pia kubeba taji la Ligi ya Mabingwa mnamo 2020.

Hata hivyo, katika mahojiano na L’Equipe, Pavard alipendekeza anaweza kuwa yupo tayari kubadilisha mazingira na kutafuta changamoto mpya akisema: “Nina heshima kubwa kwa Bayern, nilijifunza mahitaji ya kiwango cha juu sana, na ni heshima kuvaa jezi hii.”

Pavard Anaweza Kuondoka Bayern Baada ya Kombe la Dunia

Mchezaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa hakujawa na mijadala maalum kwasasa anaangazia Kombe la Dunia, pia kwanini asitamani utamaduni mpya? lakini mradi wa michezo lazima uwe wa kuvutia na hataondoka bure.

Beki huyo wa pembeni alikuwa na mchango mkubwa Ufaransa iliposhinda Kombe lao la pili la Dunia mwaka wa 2018, lakini maandalizi ya Les Bleus kwa ajili ya kutetea taji hilo nchini Qatar yamekumbwa na matatizo.

Pavard Anaweza Kuondoka Bayern Baada ya Kombe la Dunia

Ufaransa iliepuka kwa chupuchupu kushushwa daraja kutoka kwa kiwango cha juu cha Ligi ya Mataifa baada ya kupoteza mechi tatu kati ya sita katika Kundi A1 mwaka huu, lakini Pavard hana wasiwasi wowote kuhusu fomu ya timu hiyo kabla ya Kombe la Dunia.

“Sina wasiwasi. Ni bora kuwa na matatizo kabla ya mashindano makubwa kuliko wakati wa mashindano, una timu yenye wachezaji wapya wapya waliowasili hivi punde, ni kawaida kuhitaji muda.”


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa