Washambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez pamoja Edson Cavani wanajiandaa kucheza michuano ya kombe la dunia kwa mara ya nne kila mmoja, Baada ya kuitwa kwenye kikosi hicho kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Edson Cavani ambae alikua ana hatihati ya kutokuitwa kwenye kikosi hicho kwani mchezaji huyo amecheza mchezo mmoja tu ndani ya msimu huu akimaliza dakika 90,Lakini katika kikosi kilichoitwa mapema leo mchezaji huyo atakuepo kwenye kikosi cha Uruguay kitakachoenda Qatar.suarezLuis Suarez nae amejumuishwa kwenye kikosi akiwa na umri wa miaka 35 licha ya kucheza katika ligi daraja la kwanza nchini Uruguay katika klabu yake ya Nacional, Lakini kocha wa timu hiyo amemuita kutokana na uwezo ambao amekua akiuonesha kwenye kikosi hicho pale anapokua anaitwa.

Washambuliaji wote hao magwiji wote wenyre umri wa miaka 35 watakwenda kwenye michuano yao ya nne ya kombe la dunia baada ya kua pamoja mwaka 2010,2014,2018 huku Qatar ikiwa ni wazi itakua michuano yao ya mwisho wakiwa na jezi ya timu hiyo.suarezTimu ya taifa ya Uruguay licha ya kua na wakongwe kama Suarez, Cavani, pamoja na Godin lakini pia itakua namchanganyiko wa vijana wanaofanya vizuri kwenye ligi mbalimbali barani kama Federico Valverde kutoka Real Madrid pamoja Darwin Nunez kutoka klabu ya Liverpool.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa