Familia ya kifalme ya Qatar inaishinikiza FIFA kupiga marufuku kabisa uuzaji pombe katika viwanja vyote vya Kombe la Dunia, siku mbili pekee kabla ya michuano hiyo kuanza.

Taifa mwenyeji, ambapo mauzo ya pombe kwa kawaida huzuiliwa kwa wageni wanaokunywa katika hoteli na migahawa yenye leseni, au wakazi wasio Waislamu wenye vibali maalum majumbani mwao, wameweka shinikizo kubwa kwa FIFA kuacha kuuza bia katika viwanja vinane vya Kombe la Dunia.

 

fifa

Ikiwa hilo litatekelezwa itamaanisha Kampuni ya Budweiser, mmoja wa wafadhili wakubwa wa mashindano, haitaweza kuuza bia yake kwa mashabiki kwenye michezo na inaweza kuifanya FIFA kukiuka mkataba wa mamilioni ya dola na kampuni hiyo.

Majadiliano kuhusu suala hilo yanaaminika kuwa yanaendelea kati ya Budweiser na FIFA, ingawa The Times inasema kuondolewa kwa mauzo ya Budweiser sasa kuna uwezekano baada ya familia ya kifalme ya Qatar kuingilia kati. Gazeti la New York Times lilisema uingiliaji huo ulifanywa na Sheikh Jassim bin Hamad bin Khalifa al-Thani, kaka wa mtawala wa Qatar.

Kwa hali ilivyo, wageni wa Kombe la Dunia wanaweza kununua pombe katika hoteli na migahawa, katika maeneo ya mashabiki kwa nyakati fulani, na kwenye viwanja vya michezo, lakini si ndani. Bia itagharimu karibu paundi 12 katika kumbi rasmi, na mashabiki watatakiwa kutumia chini ya vinywaji vinne ili kuwazuia kulewa. Yeyote anayelewa anaweza kupelekwa katika eneo maalum ili kuwa na kiasi.

 

fifa

FIFA tayari wametoa makubaliano wiki hii kwa wenyeji wa Qatar kuhusu upatikanaji wa Budweiser katika viwanja vya michezo.

Waandaaji walisisitiza kwamba viwanja vya Budweiser vilikuwa vikionekana sana, kwa hivyo FIFA ilikubali kuwahamishia katika nafasi ambazo hazitaonekana sana. Mabadiliko kama haya si ya kawaida sana karibu na kuanza kwa mashindano.

Miezi mitatu tu iliyopita, FIFA pia ilikubali kusogeza tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo siku moja mapema ili wenyeji wacheze mechi pekee siku hiyo. Qatar v Ecuador sasa itachezwa Novemba 20.


FIFA

Kombe la Dunia linatimua vumbi huko Qatar ni Timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea.
Uwanja wa Machaguo Spesho ni kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa