Klabu ya Ruvu Shooting inatarajia kuikaribisha Simba hapo kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 jioni kwenye mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC Primia Ligi.

 

Ruvu Shooting Kukipiga Dhidi ya Simba Kesho

Ruvu Shooting ambao bado wanajikongoja kwenye ligi wana hali mbaya kwenye msimamo baada ya kuwa na mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 13 baada ya michezo 12 ambayo wamecheza.

Ruvu Shooting ndani ya hiyo michezo waliyocheza wameshinda michezo mitatu, sare mbili na wamepoteza michezo saba huku wakijivunia alama 11 pekee ambazo bado hazitoshi kuwaweka salama.

Simba wao wapo nafasi ya 3 baada ya ushindi mwembamba walioupata mechi iliyopita, huku wakiwa wamecheza mechi 11 kwenye Ligi, wameshinda mechi saba, wameenda sare mara tatu na wamepoteza mchezo mmoja mpaka sasa.

Ruvu Shooting Kukipiga Dhidi ya Simba Kesho

Simba wamejivunia pointi 24 mpaka sasa wakiwa nyuma alama mbili dhidi ya kinara wa ligi hiyo Yanga ambae ndiye bingwa mtetezi wa Ligi mwenye pointi 26 na mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi 5 za mwisho ambazo Ruvu amekutana na Simba ameshinda mechi moja pekee akipata sare moja na kupoteza mechi tatu. Je Kesho atafanya nini katika Dimba la Mkapa? Ataondoka na alama 3?

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa