SIMBA KAZI INAENDELEA

Benchi la ufundi la Simba linaendelea na maandalizi kwenye kikosi hicho kwa mechi za kitaifa na kimataifa ambapo Simba kwenye anga la kimataifa ipo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imetinga hatua ya makundi.

SIMBA KAZI INAENDELEA

Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kikosi kipo kazini kwa maandalizi ya mechi zijazo ambapo kitakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji ugenini kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Ikumbukwe kwamba Simba ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 na wanaongoza kwa timu yenye mabao mengi ambayo ni 21 ikifuatiwa na Fountain Gate ambayo safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 20.

SIMBA KAZI INAENDELEA

Fadlu amesema kuwa wanachofanya ni kufanyia kazi makosa kwenye mechi zilizopita ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo kutokana na ushindani uliopo kitaifa na kimataifa.

“Makosa yaliyopita tunafanyia kazi na malengo ni kuona tunakuwa kwenye mwendo mzuri, ninawapongeza wachezaji kwa namna ambavyo wanafuata maelekezo na kufanya kazi kwa umakini kwenye mechi zetu.”

Acha ujumbe