Klabu ya Simba hii leo majira saa 10:00 katika saa za Afrika Mashariki inatarajia kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Al Dhafra inayoshiriki ligi kuu ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

 

Simba Kucheza Mechi ya Kwanza Dhidi ya Kibonde wa Ligi ya Uarabuni Leo

Baada ya hapo Simba itacheza siku ya Jumapili mchezo wake wa pili dhidi ya SCKA Moscow ya Urusi kabla ya kurejea Jijini Dar es salaam kwaajili ya mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mbeya City.

Al Dhafra katika ligi yao ndiyo inayoshikilia mkia ikiwa nafasi ya 14, baada ya kucheza mechi zake 12 na kufanikiwa kushinda mechi moja pekee, na kutoa sare moja pekee lakini akipoteza mechi 10 zilizobaki.

Simba Kucheza Mechi ya Kwanza Dhidi ya Kibonde wa Ligi ya Uarabuni Leo

Timu hiyo imepoteza mechi nane mfululizo kwenye Ligi hiyo na kujikusanyia pointi zake 4 akiwa amefunga mabao 12 na kuruhusu mabao 36 kuliko timu yoyote katika ligi hiyo. Kinara wa ligi hiyo ni Al Sharjah akiwa na pointi 26.

Wakati kwa mgeni Simba yeye yupo nafasi ya pili akiwa na pointi 44, baada ya michezo 19, pointi 6 nyuma ya kinara wa Ligi Yanga.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa