Wakati kikosi cha Simba kikiwa nchini Dubai kujiandaa na michuano mbalimbali ambayo inawakabili, kikosi hicho kitacheza michezo miwili ya kirafiki.

Michezo hiyo ya kirafiki itakuwa dhidi ya Al Dhafra inayoshiriki ligi ya Dubai na CSKA Moscow inayoshiriki ligi kuu nchini Urusi.

Simba kucheza mechi mbili Dubai

Mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Al Dhafra utapigwa Januari 13 mwaka huu, saa 10:00 jioni huku ule wa CSKA Moscow ukitarajiwa kupigwa Januari 15 mwaka huu.

Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, raia wa Brazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kinaendelea na mazoezi nchini humo.

Simba kucheza mechi mbili Dubai

Akizungumzia hali ya kambi yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema “Kikosi kinaendelea na mazoezi na kila kitu kipo shwari kambini.

“Tutacheza michezo miwili ya kirafiki tukiwa hapa nchini Dubai kama tulivyoweka wazi na mchezo wa kwanza kocha amechagua timu hiyo ili aangalie mapungufu yaliyopo kwenye kikosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa