SIMBA NI MWENDO WA UBINGWA TU

UONGOZI wa Simba umetamba kuwa kwa sasa unawaza kutwaa ubingwa wa ligi kuu na Kombe la FA mara baada ya kuanza na Ngao ya jamii kwa kuwafunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 3-1.

Simba msimu uliopita walishindwa kubeba taji lolote tofauti na msimu huu ambapo tayari wameanza na Ngao ya Jamii ambapo msimu uliopita taji hilo lilibebwa na Yanga.SIMBAMeneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa baada ya kuanza kutwaa Ngao ya Jamii kwa msimu huu sasa kinachofuatia ni kuhakikisha kuwa wanabeba mataji yote ya ndani ambayo waliyakosa misimu miwili iliyopita.

“Msimu huu umekuwa msimu mzuri kwetu kwa kuwa tayari tumeshaanza na kutwaa Ngao ya Jamii tena kwa kumfunga mtani wetu Yanga kwa kweli sisi tunajisikia raha kwa kuwa ni mshindani wetu na tayari tumemuangusha.SIMBA“Simba kwa kiashiria hiki kwa kuanza na neema kubwa mwanzo tu wa msimu basi tuwaambie kuwa makombe mengine ya ndani ambayo tuliyapoteza tutayarudisha kwa kasi kubwa sana, Simba ya msimu huu ni mwendo tu wa makombe,” alisema kiongozi huyo.

Acha ujumbe