YANGA BILA MDAKA MISHALE GOLINI LEO

Golikipa nambari moja wa Klabu ya Yanga Djigui Diarra imethibitishwa ataukosa mchezo wa Ligi ya NBC Tanzania bara dhidi ya Coastal Unioni utakaopigwa Shekh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha leo.

YANGA BILA MDAKA MISHALE GOLINI LEO

Diara ataukosa mchezo huo kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano ambazo alizipata kwenye mechi tatu mfululizo.

Msemaji wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe ameeleza hayo jijini Arusha katika mazoezi ya Mwisho ya Yanga jana jioni na akisema kuwa makipa wawili Abou Mshery na Khomeni Abubakary watakuwa kwenye mchezo huo.

Young Africans ndio timu pekee ambayo imeshinda mechi zake zote kwenye ligi akikusanya pointi zake 18 hadi sasa huku akiwa na nafasi kubwa ya kushinda kwenye mechi ya leo akipewa ODDS 1.33 kwa 8.23.

YANGA BILA MDAKA MISHALE GOLINI LEO

Mara ya mwisho kukutana timu hizi kwenye ligi, vijana wa Gamondi waliondoka na ushindi mwembamba. Je leo hii Wagosi wa Kaya wanaweza kuwazuia mabingwa hawa watetezi wa ligi kuondoka na ushindi?

Acha ujumbe