Hatimaye ile tarehe 26 iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ikafika bhana ambapo kulikuwa na mchezo mkali sana kule LALIGA ambao ulikuwa ni EL Clasico kati ya Real Madrid vs Barcelona Yamal akipeleka moto haswa.

Mchezo huo ulipigwa majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, katika dimba la Santiago Bernabeu ambapo Barcelona chini ya kocha mkuu Hans Flick wakiibamiza Madrid ya Ancelotti bila huruma nyumbani kwao.
Ni mechi ambayo baadhi ya watu wengi waliaamini kuwa Real anaenda kushinda kutokana na usajili mkubwa ambao ameufanya ikiwa ni pamoja na kumleta mshindi wa Kombe la Dunia 2018 bwana mdogo Kylian Mbappe lakini mambo hayajakuwa kama ilivyotarajiwa hapo jana mpaka dakika 90 kukamilika.
Walienda mapumziko wakiwa 0-0 na ndipo sasa waliporeje mechi ikawa ni kali haswa kwani Robert Lewandowski alianza kufungua ukurasa wa mabao dakika ya 54 na 56, lakini pia baadae dakika ya 77 Yamal aliingia kambani na kufanya mabao kuwa 3 na mwisho kabisa Raphina alimaliza kwa kufunga la 4.



