Manchester United katika mchezo wa kombe la Carabao Cup wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao matano kwa mawili dhidi ya klabu ya Leicester City ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kocha Ruud Van Nistelrooy kama kocha msaidizi wa klabu hiyo.
Manchester United wameonesha utofauti mkubwa katika mchezo wa jana ikiwa ni mchezo wa kwanza tu baada ya aliyekua kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ambaye alifukuzwa kazi mapema jumatatu ya wiki hii baada ya kupoteza dhidi ya klabu ya West Ham jumapili iliyomalizika.Kocha Ruud Van Nistelrooy ameiongoza klabu hiyo ambayo amewahi kuitumikia kama mchezaji na kufanikiwa kuhakikisha klabu hiyo inapata matokeo ya ushindi, Klabu ya Man United jana walionekana kufufuka na kupata ushindi wa mabao matano jambo ambalo limekua adimu kwa klabu hiyo.
Klabu ya Manchester United imefanikiwa kushinda mabao matano kwa mara ya kwanza kwa timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 2021, Hii inaonesha kwa kiwango kikubwa kocha Ruud Van Nistelrooy amefanikiwa kuanza vizuri ndani ya timu hiyo huku akitarajiwa kuiongoza timu hiyo michezo mingine mitatu mbele ambayo ni kati ya Chelsea, PAOK, pamoja na Leicester wakati wanamsubiri Ruben Amorim kukabidhiwa timu.