Tchouameni Kupigwa Bei Madrid

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga ndani ya klabu ya Real Madrid Aurelien Tchouameni inaelezwa klabu hiyo ipo tayari kupokea ofa kumhusu kiungo ambaye anaonekana kupelea ndani ya klabu hiyo mpaka sasa.

Tchouameni amekua hana mfululizo wa kiwango bora ndani ya kikosi cha Real Madrid lakini pia majeraha yamekua yakimuandama mara kwa mara, ikielezwa huenda ni moja ya vitu vinavyomrudisha na kushindwa kuonesha ubora wake ambao amekua nao ndani ya klabu ya Monaco kwa misimu kadhaa nyuma.TchouameniInaelezwa klabu ya Real Madrid ipo tayari kumuamini kiungo mwingine wa kimataifa wa Ufaransa Eduardo Camavinga na kumuachia kiungo huyo wa zamani wa Monaco kutimka klabuni hapo, Hii itategemea na ofa ambayo itakuja mezani kwa mabingwa hao wa Ulaya kama itawaridhisha basi watamuuza.

Vilabu kadhaa nchini Uingereza kama Liverpool, na Man United walikua wakimfuatilia kiungo huyo kabla hajajiunga na Real Madrid, Hivo haijafahamika kama bado watakua wanavutiwa na kiungo huyo ili waweze kutuma ofa ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu na kupata hudumu ya Tchouameni.

Acha ujumbe