Klabu ya Yanga imesafiri hapo jana usiku baada ya kutua jijini Dar es saalam kutokea Tunisia walikokua wakicheza Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain na kuweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililowafanya wasonge hatua ya makundi.

 

Yanga Haipoi, Yatua Mwanza Kuwakabili Kagera

Yanga haijalaza damu baada ya kuunganisha safari kuelekea jijini Mwanza kuwakabili Kagera Sugar hapo kesho kwaajili ya mchezo wao wa Ligi kuu ya NBC unaotarajiwa kupigwa hapo kesho saa 10:00 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba.

Timu hiyo ambayo inaongozwa na Nasredine Nabi ndio mabingwa watetezi wa Ligi msimu uliopita na ndio vinara wa ligi mpaka sasa wakiwa na alama zao 20 sawa na Azam lakini yeye akiwa na michezo miwili mkononi.

Kagera sasa ina kocha mpya ambae ni Mecky Mexime aliyerejea baada ya kuondoka klabuni hapo siku si nyingi baada ya klabu hiyo kumfurusha aliyekuwa kocha wao Francis Baraza kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Yanga Haipoi, Yatua Mwanza Kuwakabili Kagera

Mara ya mwisho kukutana timu hizo, Yanga alishinda kwa mabao matatu kwa bila na sasa wanakutana tena hapo kesho huku Mecky akisema kuwa wamejiandaa kupata alama hizo hapo kesho.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa