Klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredine Nabi imebakiza kushinda mechi tisa kati ya 10 zilizobaki za Ligi Kuu ya NBC ili kutangazwa kuwa Bingwa wa msimu huu wa 2022/23.

Yanga mpaka sasa yupo nafasi ya kwanza akiwa na pointi zake 53 kwenye michezo 20 ambayo amecheza, akiwa mbele pointi 6 kwa anayemfuata nafasi ya pili ambaye ni Simba mwenye pointi 47.
Hivyo, Young Africans akishinda mechi zake atafikisha pointi 80 ambazo timu yoyote haitaweza kuzifikia pointi hizo kwenye ligi msimu huu huku kwa upande wa Simba yeye kuzifikia pointi hizo inakuwa ni ndoto.

Katika kechi hizo 10 za Mabingwa watetezi wa Ligi sita atacheza kwa Mkapa. Je wanaweza kutetea tena taji hili msimu huu na kuwa Mabingwa mara 29 wa Ligi?

