Klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka Dimbani hapo kesho majira ya saa 12:15 kukiwasha dhidi ya Coastal Union ya Tanga, baada ya kuibugiza Polisi Tanzania mabao 3-0 wakiwa uwanjani kwa Mkapa.

 

Yanga Kurejea Uwanjani Kesho Dhidi ya Coastal Union

Yanga wapo kileleni kwenye msimamo hadi sasa wakiwa wameshinda mechi zao 13 kati ya 16 walizocheza, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja wakiwa na pointi zao 41 kibindoni.

Wakati kwa upande wa Wagosi wa Kaya wao bado mambo ni magumu kutokana na mwenendo wa matokeo wanayoyapata, ambapo mechi ya mwisho wametoka kupoteza dhidi ya KMC.

Yanga Kurejea Uwanjani Kesho Dhidi ya Coastal Union

Coastal Union wameshinda michezo minne pekee kati ya 16 waliyocheza, sare tatu na kupoteza mara tisa wakijukusanyia pointi zao 15 tuu, malengo yao yakiwa ni kupambania kutoshuka daraja.

Mechi ya mwisho ya ligi kukutana Yanga na Coastal, Wananchi waliondoka na pointi tatu zote huku Wagosi wakishindwa hata kupata bao lolote.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa