Nyota wa Simba, Kibu Denis amefungua akaunti yake ya mabao jana jumapili baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo wa ligi kuu ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kibu afungua akaunti ya mabao Simba

Tangu kuanza kwa msimu huu nyota huyo hakufanikiwa kufunga bao lolote hivyo jana alifanikiwa kufunga bao hilo akitokea benchi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kibu alisema “Kwanza namshukuru Mungu kwa kufanikiwa kufunga bao langu la kwanza msimu huu.

Kibu afungua akaunti ya mabao Simba

 

“Kweli kwa upande wangu nimefurahi sana kufunga bao langu la kwanza kwa msimu huu na wachezaji wenzangu, mashabiki pamoja na benchi la ufundi nawashukuru kwa mapokezi yao.

“Msimu uliopita nilifanya vizuri hivyo msimu huu watu walitarajia nitafanya vizuri zaidi lakini haikuwa hivyo ila naahidi kufanya vizuri kwani kila kitu kina muda wake.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa