Klabu ya Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam kibabe baada ya kuichakaza Tanzania Prisons kwa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa majira ya saa 1:00 usiku katika dimba la Azam Complex.

 

Yanga Yatinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Azam Kibabe

Mabao hayo yalitupiwa kimyani na Bakari Mwamnyeto, Clemet Mzize akitupia mabao mawili, huku Aziz Ki akifunga bao moja na kukamilisha idadi ya mabao manne, wakati kwa upande wa Prisons bao la kufutia machozi lilifungwa na Jumanne Elifadhili.


Tanzania Prisons walikuwa na kadi nyekundu ambayo alipewa beki wao Abraham baada ya kucheza madhambi kwa wakati tofauti kwa wachezaji wa Yanga huku ya kwanza akimchezea Aziz Ki, na ya pili akimchezea Kisinda.

Yanga Yatinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Azam Kibabe

Na kufanya timu yao kucheza wakiwa pungufu hapo jana huku wakibugizwa mabao kibao katika dimba la Chamazi.

Baada ya kufunga mabao hayo mawili hapo jana, Mzize sasa nakuwa ndiye kinara wa ufungaji katika michuano hii ya Kombe la Azam akiwa amefikisha mabao sita hadi sasa.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa