AFCON 2021 : Egypt na Senegal Zatinga Nusu Fainali.

Wachezaji Mohammed Salah na Sadio Mane wameongoza timu zao za taifa Egypt na Senegal kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON 2021 inayofanyika Cameroon.

Mohamed Salah alifunga bao na kuchangia jingine katika ushindi wa 2-1 uliosajiliwa na Misri dhidi ya Morocco katika muda wa ziada kwenye robo-fainali ya Kombe la Afrika AFCON hapo jana.

Mechi kati ya Egypt na Morocco ilirejesha kumbukumbu za miaka mitano iliyopita ambapo Misri walitandika Morocco 1-0 katika robo-fainali za AFCON 2017 jijini Port-Gentil, Gabon.

Simba wa Teranga, Senegal waliibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Equatorial Guinea yaliyoweka wavuni na Famara Diedhiou (28′) akipokea pasi ya Mane, Cheikhou Kouyate (68′) na Ismaila Sarr (79′) wakati lile la kufutia machozi la Equatorial likifungwa na Jannick Buyla (57′).

Nusu Fainali ya kwanza itawakutanisha Burkina Faso dhidi ya Senegal siku ya Jumatano wakati ile ya pili ikiwakutanisha wenyeji Cameroon dhidi ya Egypt siku ya Alhamisi saa nne usiku.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe