Ligi kuu yaUingereza iliendelea hapo jana kwa michezo kadhaa lakini mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa ni ule wa mwenyeji Arsenal dhidi ya bingwa mtetezi Manchester City ambao ulimalizika kwa vijana wa Pep Guardiola kupokea kichapo cha mabao 5-1.
Arsenal na City wote wapo kwenye mbio za ubingwa huku timu hizi zikitofautiana pointi 6 pekee ambapo mechi ya kwanza walitoa sare pale Etihad huku jana ambaye alikuwa anapewa nafasi ya kushinda alikuwa ni The Gunners kwani faida yao ya kuwa nyumbani ndiyo ambayo ilifanya apewa ODDS kubwa ya kushinda.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Mpaka kufikia dakika 45 za kwanza Arteta na vijana wake walikuwa wapo mbele kwa bao 1 ambalo lilifungwa na Odegaard huku wakipeleka mashambulizi makali sana kwenda kwa vijana wa Pep Guardiola.
Baada ya kipindi cha pili kuanza dakika ya 55 Erling Haaland aliweza kusawazisha bao hilo, lakini Arsenal bado walikuwa na kibarua cha kuwapa furaha mashabiki wao ambao walikuja uwanjani kuutazama mchezo huo wakiwa na matarajio makubwa ya ushindi hasa ukizingatia kuwa City bado haiko kwenye hali nzuri.
Thomas Partey kiungo maridadi kabisa hakuweza kumpa Haaland nafasi kubwa ya kushingilia goli lake, kwani dakika ya 56 alifunga bao la pili la uongozi la kwa Arsenal.
Lakini pia mtoto mdogo kabisa kutoka kwenye Academy ya The Gunners Lewis Skelly aliingia kambani na kufunga bao lake la kwanza kama mchezaji wa timu hiyo inayoongozwa na Arteta, naye Havers alifunga bao la 4 huku dakika ya 93 Nwaneri aliimaliza Arsenal kabisa kwa kufunga bao la 5.
Mechi inayofuata ya ligi The Gunners watakipiga dhidi ya Leicester City ugenini, huku City wao watakuwa nyumbani kusaka ushindi wao dhidi ya Newcastle United.