IBRA BACCA ANAWAKALISHA

Beki wa kati ndani ya kikosi cha Yanga kinachofundishwa na Sead Ramovic, Ibra Bacca amewafunika mabeki wote Bongo kwenye rekodi za kuwa na ushkaji na nyavu kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi licha ya kwamba yeye ni mlinzi.

IBRA BACCA ANAWAKALISHA

Kutoka Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC ambayo ni namba nne kwa ubora barani Afrika, Ibrahim katupia mabao manne kwenye ligi na kinara wa utupiaji ni Elvis Rupia wa Singida BlacK sTARS huyu ni mshambuliaji kafunga mabao 8.

Anashikilia rekodi ya kufunga bao lililopewa jina la mkono wa ajabu ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo huo Bacca alitupia mabao mawili.

Ilikuwa ni Desemba 22 2024 mchezaji huyo alifunga mabao hayo ilikuwa Uwanja wa KMC, Complex bao la kwanza alifunga dakika ya 42 na bao la pili la mkono wa maajabu alifunga dakika ya 83.

IBRA BACCA ANAWAKALISHA

Timu ya kwanza kufungwa na Bacca msimu wa 2024/25 ni Ken Gold mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine ilikuwa dakika ya 14 kwa pigo la kichwa na bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huku timu ya pili kufungwa ikiwa ni Pamba Jiji, ilikuwa Oktoba 3 2024, Uwanja wa Azam Complex.

Bacca amecheza mechi 10 za ligi ameyeyusha dakika 747 ni chaguo la kwanza la Sead ambaye ni kocha mkuu wa Yanga iliyogotea hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Acha ujumbe