GARI LA MPANZU LIMEWAKA

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ellie Mpanzu ameanza kuonyesha ujuzi wake kwenga anga la kimataifa kutokana na kuandika rekodi ya kutoa pasi yake ya kwanza akiwa na uzi wa mnyama ilikuwa ni katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Mkapa hatua ya makundi.

GARI LA MPANZU LIMEWAKA

Ikumbukwe kwamba Mpanzu bado hajawa fiti asilimia 100 kutokana na kukaa muda mrefu bila kucheza lakini ameanza kupata namba kikosi cha kwanza cha Simba kinafundishwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Kwenye mechi za ligi ambazo alipata kucheza ambazo ni tatu akikomba dakika 186 hakupata zali la kufunga wala kutoa pasi ya bao na ikumbukwe kwamba mchezo wake wa kwanza kuwa uwanjani ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa kaiataba.

Katika mchezo huo Simba iliandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa ndani ya ligi namba nne kwa ubora baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 2-5 Simba.

Kwenye mchezo dhidi ya Constantine ambao ulikuwa ni wa hatua ya makundi alipofungua akaunti yake ya pasi za mwisho ilikuwa dakika ya 61 akitumia pasi mpenyezo kutoka kwa Fabrince Ngoma akaitoa kwa Kibu Dennis aliyefunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo.

GARI LA MPANZU LIMEWAKA

Mpanzu amezidi kuimarika taratibu akiwa na uzi wa Simba kwenye mechi za ushindani huku akiweka wazi kuwa furaha kubwa ni kuona timu hiyo imetinga hatua ya robo fainali.

Simba inaongoza Kundi A baada ya mechi 6 imekusanya jumla ya pointi 13 kibindoni ikiwa imetinga hatua ya robo fainali katika anga la kimataifa.

Acha ujumbe