Azam FC : Amoah Aongeza Miaka 2 Chamazi.

 

Beki kisiki wa Azam FC, Daniel Amoah, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili zaidi kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.

Amoah amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin β€˜Popat’ jana Alhamisi.

Mkataba huo mpya utamfanya Amoah kubakia Chamazi hadi Agosti 2024, ambapo ule wa awali ulikuwa unamalizika utakapoisha msimu huu Julai 31, 2022.

Beki huyo raia wa Ghana amekuwa na kiwango kizuri katika eneo la ulinzi la beki wa kati tokea ajiunge na klabu hiyo Agosti, 2016 akitokea Medeama ya nchini kwao.

Msimu huu amefanikiwa kucheza mechi zote tisa za mashindano yote, akifanikiwa kufunga bao moja, Azam FC ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.