Kiungo wa zamani wa Hertha Berlin, Tottenham na AC Milan, Kevin-Prince Boateng ameweka wazi alikataa kujiunga na klabu ya Manchester United miaka 8 iliyopita na kujiunga na Schalke.
Boateng, 34 alijiunga Ligi ya Bundesliga mwezi wa nane mwaka huo mpaka majira ya joto mwaka 2017 ambapo mkataba wake ulisitishwa ikiwa ni baada ya miaka miwili na nusu baadae.
Mchezaji huyo anasema anajuta kuacha nafasi ya kujiunga na Manchester United ipite na kujiunga na Schalke kwani kipindi kifupi alichokaa AC Milan alikua kama mchezaji.
“Nilikua na nafasi ya kujiunga Manchester United. Nilichagua Ujerumani – mlione kilichonitokea nikiwa Schalke,” alisema kwenye tovuti ya Hertha.
“Kwa muda fulani nikua kiakili. Ilianza nikiwa Milan. Nilicheza na wachezaji wenye viwango vya dunia na nilijifunza kitu kwa kila mtu.”
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


