Baada ya kuondolewa katika michuano ya Europa League, Meneja wa Leicester City, Brendan Rodgers amesema hafahamu kuhusu mashindano mapya ya Europa Conference League ambayo wanaweza kucheza huko.

Leicester City walipoteza jana kwa magoli 3-2 mbele ya Napoli katika michuano ya Europa League, na kushika nafasi ya tatu katika kundi na sasa atacheza hatua ya mtoano katika michuano mipya ya Europa Conference League.
“Lazima niwe mkweli, Sijui hata hayo mashindano yanahusiana na nini. Nilikuwa nimejikita kwenye Ligi ya Europa na kuongoza kundi.
“Na kwa kiasi, kumaliza nafasi ya pili, kwahiyo kwa kuheshimu mashindano, Sina uhakika yanahusiana na nini. Natarajia kujua hilo haraka iwezekanavyo.” aliongeza Rodgers.
Katika mashindano hayo West Ham ya EPL imefanikiwa kusonga mbele licha ya kupoteza katika mchezo wake wa mwisho nyumbani dhidi ya Dinamo Zagreb.
Leicester City ataungana na Tottenham anayeshiriki michuano ya Europa Conference League endapo atafanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.
CHEZA HAPA


