Chelsea Kurudi kwa Alvarez Tena

London: Timu ya Chelsea wanapanga kutumia pesa wakati wa mauzo ya wachezaji dirisha dogo yatakayofanyika  mwezi Januari ambapo Chelsea walifanya harakati kadhaa za dakika za mwisho kwa viungo kabla ya dirisha la majira ya joto kufungwa wiki iliyopita akiwemo Alvarez

Chelsea Yashinikiza Kumnunua Alvarez

 

Na mwishoni Denis Zakaria ndio walifanikiwa kumchukua tena ikiwa kwa mkopo kutoka Juventus wakati kwa upande wa Edson Alvarez wa Ajax, na Romeo Lavia wa Southampton hayakufanikiwa.

Alvarez anaripotiwa kuwa kinara wa orodha wa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel licha ya ofa ya pauni milioni 40 kukataliwa na Ajax. Vilevile kwa upande wa mchezaji huyo aliwafahamisha mabingwa hao wa Eridivisie kuhusu nia yake ya kuhamia Uingereza  lakini akagundua kuwa klabu yake haitaki kumwachia aondoke baada ya timu hiyo kumpoteza Antony ambae kaenda Manchester United.

 

Chelsea Yashinikiza Kumnunua Alvarez

Mbali na Alvarez na Lavia ripoti hiyo inadokeza kwamba Chelsea itamnunua mchezaji wa kimataifa wa Urusi  Arsen Zakharyan. Kiungo huyo wa Dinamo Moscow(19)  anafuatiliwa na klabu nyingi kubwa  za Ulaya .

Ilionekana kutowezekana kumleta kinda huyo wakati wa dirisha la majira ya kiangazi kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Urusi  lakini The Blues watajaribu tena Januari kama hali itaruhusu. Kipengele cha pauni milioni 12.6 kinamaanisha kuwa dili linapaswa kuwa rahisi kufikiwa ikiwa mchezaji ana nia ya kuhamia Stamford Bridge.

Chelsea Yashinikiza Kumnunua Alvarez

Acha ujumbe