Golikipa wa Chelsea Edouard Mendy, ameendelea kuweka historia na rekodi katika klabu yake baada ya kuwa kipa wa kwanza kucheza mechi nyingi za Klabu Bingwa bila kufungwa.

 

chelsea, Chelsea, Mendy Kwenye Rekodi Mpya., Meridianbet

Baada ya kuichapa Lille 2-0 katika mkondo wa kwanza 16-bora wa michuano hiyo ya bara Ulaya, Mendy amecheza mechi 14 bila kufungwa katika mechi 18 alizocheza.

Mbali na kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa barani Ulaya, kadhalika kipa huyo aliisaidia timu yake ya taifa kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) pamoja na ubingwa wa FIFA Club World Cup akiwa na Chelsea mapema mwezi huu.

Ushindi dhidi ya Lille ambao ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa umewaweka katika nafasi nzuri ya kuwa na kazi rahisi katika mechi ya marudiano itakayochezwa Machi 16 ugani Stade Pierre-Mauroy.

Chelsea pia wameweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutoka Uingereza kucheza mechi 8 nyumbani bila kupoteza wala kufungwa goli katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa