Klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga imemtangaza kocha wake mpya Yusuf Chipo kwa mkataba wa mwaka mmoja kufuatia aliyekuwa kocha wao mkuu Juma Mgunda  kutimkia katika klabu ya wekundu wa msimbazi Simba.

 

Coastal Union Yamtamtangaza Chipo

Coastal wamemtambulisha kocha huyo aje kuitumikia klabu hiyo kwa msimu huu kwani baada ya kuondoka kwa Mgunda hawakua na mwalimu na ligi imeshaanza sasa. Mgunda ameitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu sasa ambapo ndani ya hiyo misimu ameweza kuifikisha Coastal kucheza fainali ya michuano ya Azam Federation Cup.

Fainali hiyo ilipigwa huko Arusha msimu uliopita ambapo kwenye hatua ya nusu fainali alimtoa Azam katika hatua ya mikwaju ya penati, na ndipo wakakutana na Yanga kwenye hatua ya fainali ambapo mechi ilikuwa ngumu kwelikweli na kuisha tatu kwa tatu katika dakika za 90 na zilipoongezwa dakika za nyongeza 30 Coastal alipoteza mchezo huo.

 

Coastal Union Yamtamtangaza Chipo

Chipo anaichukua timu hiyo ikiwa imecheza mechi tatu kwenye ligi kuu ya NBC ambapo imeshinda mechi moja, imetoa sare moja na imepoteza mechi moja huku ikiwa katika nafasi ya tisa kwenye msimamo na mechi ijayo atakuwa ugenini akicheza dhidi ya Namungo ya mkoani Lindi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa