Kocha mkuu wa Tottenham Hott Spurs  Antonio Conte amesema kuwa anaamini itakuwa ni bora zaidi kama watakuwa wanambadilisha Son Heung-Min badala ya kuwa nyota mshambuliaji ambaye atakuwa anaanza kila mchezo.

 

Conte Kumpumzisha Son

Son Heung Min  amecheza angalau mechi 40 katika mashindano yote kwenye kila misimu yake saba akiwa Spurs wakati katika kampeni yake ya kwanza tu huko England alianza chini ya mechi 30. Msimu huu mshambuliaji huyo wa Korea Kusini ameanza mechi zote saba za klabu yake ingawa bado hajafunga ila ametoa pasi  moja pekee ya goli.

Huku Richarlison akisajiliwa mwishoni mwa msimu, kufuatia kuwasili kwa Dejan Kulusevski Januari, Conte anaonekana sasa kumuacha Son nje ya timu kutokana na hiyo fomu aliyonayo sasa.

 

Conte Kumpumzisha Son

Conte anaweza kufanya hivyo akiwa na Sporting CP ugenini hii leo kwenye ligi ya mabingwa ingawa kuahirishwa kwa mchezo wikendi iliyopita dhidi ya Manchester City kutokana na kifo cha Malkia Elizabeth wa pili kumeipa zaidi timu yake muda wa kujiandaa vizuri, huku akijaribu kuwaweka sawa Son, Richarlison, Kane na Kulusevski kwenye XΙ, huku akisema kuwa mechi iliyoahirishwa inaniruhusu kufanya uamuzi tofauti.

“Dhidi ya Manchester City ningecheza na wachezaji fulani, Lakini sasa ninabadilisha mambo katika akili yangu”

 

Conte Kumpumzisha Son

Kocha huyo alipoulizwa kama anaweza kumuacha Son alijibu kuwa, “Unapojaribu kujenga kitu muhimu kwa matamanio, na kujaribu kuwa mshindani na kushinda, lazima ubadilishe tabia za zamani-vinginevyo ubaki na usawa na hutakiwi kuwa na tamaa”

Kwahiyo wachezaji wote wanapaswa kukubali kwamba mzunguko ni sehemu ya kipengele hiki. Tuna wachezaji wanne mbele na hivyo ni vigumu hivi sasa kumuacha mmoja. Lazima nichukue uamuzi bora wakati mwingine kwa wachezaji. Wakati mwingine ni bora kuingia kwa dakika 20, 30 kwaajili yao. Kwasasa hatuna kikosi kikubwa, Lakini ndio tumezanza mchakato huu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa