Barcelona,Bayern wanakutana katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa huku timu zote zikiwa zimeshinda michezo ya awali wa ligi ya mabingwa ulaya mchezo utakaopigwa katika dimba la Allianz Arena.

Bayern wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kusuluhu michezo mitatu mfululizo wa wa ligi kuu Ujermani maarufu kama Bundesliga kitu ambacho kinaweza kuwaathiri kiakili kuelekea mchezo ambao wanakutana na Fc Barcelona iliopo kwenye ubora mkubwa ambapo mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote walioingia uwanjani.

barcelonaMechi hii pia inatazamiwa pia kama ya kisasi hasa kwa klabu ya Barcrlona ambao wamekua wakipata vipigo vizito dhidi ya Bayern miaka ya karibuni hivo kuelekea mchezo huu inaweza kua nafasi ya Barca kufanya maajabu baada ya kuanza vizuri msimu huu na kua kwenye kiwango bora kabisa.

Mchezo huu unakwenda kuvuta hisia za watu wengi pia pale nyota wa zamani wa klabu ya Bayern Roberto Lewandowski ambae atarudi kwenye dimba la Allianz Arena akiwa na klabu yake mpya ya Barca na watu wengi kusubiri je atawaadhibu waajiri wake hao wa zamani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa