Chama cha soka cha Wales (FAW) kimetangaza kuwa meneja wa timu ya Taifa hilo Rob Page ametia saini ya kuitumikia timu hiyo kwa muda wa miaka minne. Kombe hilo linatarajia kufanyika huko Qatar November mwaka huu.

 

Wales Yampa Mkataba Mpya Rob

Page alichukua nafasi ya bosi  kama mlezi wa Wales mnamo Novemba 2020, kufuatiwa Ryan Giggs kukamatwa kwa tuhuma za unyanyasaji na kupelekea timu hiyo kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 64.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 pia aliisaidia Wales kutinga hatua ya 16 bora kwenye Euro 2020 na kupata kufuzu kwa Mataifa A kwa mara ya kwanza. Giggs alijiuzulu mwezi Juni, huku page akichukua wadhifa wa kudumu ndani ya timu hiyo.

 

Wales Yampa Mkataba Mpya Rob

Na FAW wamemlinda kocha huyo kwa kuamua kumpa mkataba wa muda mrefu  kwa nia ya kampeni zao za kufuzu kwa Euro 2024  na kombe la Dunia la mwaka 2026. Kocha huyo alisema kuwa;

“Hakuna heshima kubwa zaidi ya kufundisha timu yako ya Taifa na siwezi kusubiri changamoto ambayo itakuja miaka minne ijayo, kuanzia na kombe letu la kwanza la FIFA la Dunia katika miaka 64”

Page alisema kuwa huu ni wakati wa kusisimua kwa Wales, na ninatumai tunaweza kufanya nchi kujivunia mnamo Novemba na kuendeleza mafanikio yetu kwa kufuzu mashindano makubwa zaidi siku zijazo, ambapo Wales wamepangwa kundi moja na Uingereza, Marekani na Iran katika kombe la Dunia huko Qatar.

 

Wales Yampa Mkataba Mpya Rob

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa