Wales imeafnikiwa kufuzu kushiriki kombe la Dunia 2022 nchini Qatar baada ya kufunga Ukraine 1-0 siku ya Jumapili katika mchezo wa mchujo ambao ulicheleweshwa sababu vita inayoendlea nchini Ukraine.

Imepita miaka 64 tangu Wales wacheze michuano ya Kombe la Dunia mara ya mwisho ilikuwa kombe la Dunia la mwaka 1958.

Goli la kujifunga la Andriy Yarmolenko ambaye alikuwa akijaribu kuokoa mpira uliyopigwa na Gareth Bale lilitosha kuivusha Wales ambao walikuwa wakiota kila mara kushiriki michuano hiyo mikubwa katika ulimwengu wa soka.

“Ni matokeo bora zaidi katika historia kwa soka la Wales,” Bale aliambia Sky Sports. “Sote tuna furaha. Mashabiki kwa pamoja, ilikuwa furaha, na tunaenda kwenye Kombe la Dunia!

“Inamaanisha kila kitu. Ndivyo ndoto zinatimizwa. Ndio tumekuwa tukifanya kazi tangu tulipokuja hapa. Nina furaha kwa mashabiki wetu wote wa ajabu na nchi yetu. Maneno hayawezi kuelezea jinsi tunavyojisikia. kwa sasa.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa