Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa mchezo wake wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya RB Salzburg uliopangwa kuchezwa kwenye dimba la Stamford Bridge siku ya Jumatano utaendelea kama ulivyopangwa.

Baadhi ya michezo ilikuwa kwenye majadiliano ya kuahirishwa kutokana ma kifo cha Malkia Queen Elizabeth II, Uwepo na upatikanajiwa hafifu wa polisi ili kulinda usalama wa michezo yote ndiyo imepelekea baadi ya michezo kuahirishwa.

Chelsea, Chelsea Yathibitisha Mchezo wake Dhidi RB Salzburg Utaendelea kama Ulivyopangwa, Meridianbet

Mchezo kati ya Arsenal vs PSV Eindhoven wa Europa League ambao ulipaswa kuchezwa siku ya Alhamisi umeahirishwa lakini Chelsea wamethibitisha kuwa mchezo wao wa ligi ya mabingwa utaendelea kama ulivyopangwa.

“Mchezo wetu wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya RB Salzburg siku ya jumatano usiku utaendelea kama ulivyopangwa.” Chelsea.

Chelsea kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Dinamo Zagreb walipoteza kwa 1-0, na kupelekea kocha wao thomas Tuchel kufangashiwa virago vyake siku moja baadae.

Graham Potter atakuwa na kibarua cha kuiongoza klabu ya Chelsea kwenye mchezo wake wa kwanza tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa klabu hiyo alitokea klabu ya Brighton.

Pia Premier League wamethibitisha mechi zote za soka kuendelea wiki hii lakini klabu ya Chelsea inaweza isicheze wiki hii.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa