MTENDAJI Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez alisema kuwa kwa mara ya kwaza timu hiyo baada ya kipindi kirefu kupita imeongozwa na makocha Watanzania kwenye mchezo wa kimataifa na kufanikiwa kupata ushindi.
Barbara alisema alichokifanya kocha Juma Mgunda na Seleman Matola wikiendi iliyopita ni kufuata maelekezo ya uongozi na kutimiza yale yote ambayo walikubaliana wayafanye akiwa katikati ya uwanja na yameonekana.
Barbara alidokeza kuwa: “Tumefurahia kuanza na ushindi tukiwa ugenini na kwa mara ya kwanza Simba SC ikiongozwa na makocha wazawa kwenye mechi kubwa ya kimataifa.
“Walichokifanya ni kutimiza makubaliano yetu na Mgunda anajua nini sisi tunahitaji na wapi tunatakiwa kufika kwenye mashindano hayo. Jambo zuri tumeona alichofanya uwanjani.
“Naamini kuwa atafika kule tunakohitaji kuanzia kwenye hatua ya makundi, robo fainali na kuvuka hadi kwenda fainali kama ambavyo kila mwanasimba anahitaji.”.Mtendaji Mkuu wa Simba.