Barbara Gonzalez Afunguka Makocha Wa Afrika.

Klabu ya Simba SC ipo kwenye mchakato wa kumpata mrithi wa Didier Gomes baada ya kuachana na kocha huyo. CEO – Barbara Gonzalez atoa neno.

Simba ilichukua uamuzi wa kuachana na Gomes muda mfupi baada ya timu hiyo kupoteza mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy na kutolewa kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kila mtu amekuwa na neno lake la kusema kwa kile kilichotokea. Uhalisia ni kwamba, maamuzi ya kuachana na Gomes yaliafikiwa na pande zote zilizohusika.

Chapisho la Barbara kupitia mtandao wa Twitter.

Kwa sasa, Simba SC ipo kwenye mchakato wa kumpata kocha mpya. Wakati mchakato huu ukiendelea, CEO wa Simba, Barbara Gonzalez ametoa neno kwa makocha wa kiafrika. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Barbara ameandika:

Makocha ndani ya bara hili (Afrika), wanapaswa kujiamini. 95% ya wasifu (CV) zilizotumwa zinatoka nje ya Afrika. Ni kwamba, makocha wetu wanaogopa changamoto au, ni hawana vigezo vya kuomba kazi hizi.

Ni kumbusho kwa klabu yenye maono ya kukuza soka la Afrika.


MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe