Bodi ya ligi kuu nchini Uingereza ‘Premier League’ wamethibitisha kuahirishwa kwa michezo miwili ya ligi hiyo kutokana na kutokuwepo polisi wa kutosha kufuatia kwa kuwepo kwa siku 10 za maombolezo ya malkia Elizabeth.
Premier League chiefs leo mchana aliongoza kikao ambacho walikuwa wanajadili hatua zingine za kuzipangia tarehe nyingine baada ya kuahirishwa kwa michezo wikiendi iliyopita.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa Chelsea vs Liverpool na Manchester United vs Leeds zilipaswa kuahirishwa kutokana na ratiba ngumu na upungusu wa polisi.
Kutokana na kuwepo kwa siku 10 za maombolezo kumekuwepo na upungufu mkubwa wa polisi kutokana wengi wao kupangiwa majukumu ya kusimamia mazishi ya msiba wa malkia Elizabeth kwenye kitengo cha usalama.
Japo mchezo kati ya Man Utd na Leeds kuchezwa kwenye dimba la Old Trafford jijini Manchester lakini polisi wengi wa jiji hilo wamehamishwa kwa dharula kuelekea nchini Scotland na London kufuatiwa kifo cha Malkia.