KIUNGO mkabaji wa Tottenham Hotspur, Eric Dier amerefusha mkataba wake kambini mwa miamba hao wa soka ya Uingereza hadi mwishoni mwa msimu wa 2024.
Dier, 26, aljiunga na Tottenham mnamo 2014 baada ya kuagana rasmi na kikosi cha Sporting Lisbon nchini Ureno kwa kima cha Sh560 milioni.

“Nafurahi sana kwamba nitakuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Tottenham katika kipindi cha misimu kadhaa ijayo,” akatanguliza Dier ambaye pia ana uwezo wa kutamba akiwa beki wa kati.
“Tottenham walinipa fursa ya kudhihirisha uwezo wangu uwanjani katika soka ya Uingereza. Wamenifanyia mengi ambayo natambua na kuthamini. Ni matarajio yangu kwamba nami nitaendelea kujitahidi na kuwatambisha katika kipindi hiki ninapovalia jezi zao,” akaongeza Dier.
“Lengo langu ni kushirikiana vilivyo na kocha pamoja na wanasoka wengine ili kushindia Tottenham idadi kubwa zaidi ya mataji ya haiba kubwa. Ningependa kuondoka Tottenham nikifahamu kwamba nimefanya yote ambayo yamo ndani ya uwezo wangu katika juhudi za kuwavunia mataji muhimu ndani na nje ya kampeni za soka ya Uingereza,”.
-Dier
Hadi kufikia sasa, kiungo huyo amewajibishwa na Tottenham katika jumla ya mechi 239 na akapachika wavuni mabao 11.
Mnamo Julai 8, 2020, Dier alipigwa marufuku ya mechi nne na kutozwa faini ya Sh5.6 milioni kwa kosa la kumvamia shabiki aliyemtusi uwanjani mnamo Machi 2020.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mechi iliyoshuhudia Tottenham wakibanduliwa na Norwich City kwenye kipute cha kuwania ubingwa wa Kombe la FA msimu huu.

Erick pia alionywa na FA kwamba atakuwa katika hatari ya kuadhibiwa vikali zaidi katika siku za usoni iwapo atarudia makosa ya sampuli hiyo.
Tukio hilo lilifanyika mnamo Machi 4 wakati wa mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA iliyoshuhudia mshindi akiamuliwa kwa mikwaju ya penalti. Licha ya mchezaji huyo kupachika wavuni mkwaju wake, waajiri wake Tottenham walipoteza mechi hiyo na hatimaye kubanduliwa nje ya kipute cha Kombe la FA.
Wakati huo, kocha Jose Mourinho alikataa kabisa kuzungumzia suala hilo, akionya kwamba Tottenham na Dier wangalijipata katika hatari ya kuadhibiwa vikali zaidi iwapo yeye angefichua msimamo wake wa kutetea kikosi chake na matendo ya mwanasoka wake huyo.
Dier anajivunia kuvalia jezi za timu ya taifa ya Uingereza katika mechi 40 za hadi kufikia sasa.
Kwa sababu ya thamani ya pesa yako, kwa kila muamala unaofanya wa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet unapata 5% bonasi.


caroline
safi sana Dier piga kazi
mwajumah
Safii sana#Meridianbettz
aisha
Dier yuko vizuri namkubali sana
Mwanahamisi
Safi sana
Khadija
Safi sana#meridianbettz
Antony Luseno
Spurs sio rahisi kumruhusu died kuondoka kwa sasa
Njiku
Safii hii inaonyesha kuwa uwongozi wa tottenham umekubali kazi yake na kumuongeza mkataba dier
Magdalena
Spurs wapo vizuri na wamefanya vyema kumuongezea mkataba maana yupo vizuri
Ester jackson
Asante kwa nakala mana hapa inaonyesha jinsi gani mchezaji mwenye matamanio anavyo taka kufanya kitu kinzuri kwenye timu aliyopo kabla hajaondoka nampongeza sana Eric dier anaipenda timu yake anataka aweke historia kuwa alifanya kitu muhimu kwa Tottenham .iko tafauti sana na kwetu Tanzania mchezaji kabla hajaonyesha mafanikio kwenye klabu yake akipata kishawishi tu kwenye klabu nyingine anaaza sababu ambazo hazina mashiko wachezaji mnapaswa kuiga mafanikio sio kuiga ufahari. #meridianbettz
Ernest
Eric Dier anakibarua cha kumfanya Mourinho azidi kumuamini kwenye kikosi chake
Dorophina
Erick yupo vizuri naona Tottenham wameamua kumuamini inabidi na yy kuonyesha kipaji chake
Samira
Hongera sana dier
Lydia Emmanuel Magoti
Safii sana
Rose kapinga
Pongez kwako dier piga kazi wakuamin Zaid uxiwaangushe
[email protected]
Safi sana piga kazi
Franky
Good news
Theckla
Inapendeza
Fatina mfingi
Makala nzur
Tahiya
Habari njema
devotha
habari nzuri sana
Isaya massawe
Dier ni mchezaj mzuri
Flomena
Waoow Good news
Gabriel
Ila kwa upande mwngne Eric dier alizingua sana kutokana na tukio ambalo alilolifanya mnamo julai 8 2020 amwaka huu kikwel n tukio la aibu sana kwa club ya Tottenham chin ya kiongoz kocha mkuu Jose Mourinho ila sio la kulizungumzia sana ila habar njema sana kwa bek huyu wa Kati kuongeza mkataba mwingine mpaka 2024 iko poa sana 👍 tunatumain alichokiongela kuhusu Hotspur miaka minne atafanya vzur kwan tunatambua uwezo wa huyu bek wa kati
Saupha mohamed
Vizurii
Furahav
Dier ni beki kisiki,anastaili kuendelea hapo spurs.
lombo
habar njema
Samiah
Habari moto moto
Povel
Habar njema
Zuhura omary kindamba
Habali njema kwetu mashabiki
Amiri Kayera
Ni vizur
Johnmary joel
Hongera zako#meridianbett
Janeflora malisa
Vzr
Theonestina
Saafi sana
Genia Sikaluzwe
Good 👍 news
Omary lukumbi
Safi sana
tumaini
Maoni:safi
Neema juma
Hiyo ndo safi sana
Zeiyana
Dier amekua na humuimu kubwa sana pale Tottenham
Tatu
Habari nzuri
Amani
Safi Sana kwa Tottenham kumuongezea mkataba dier Ni mchezaji mzuri sana #meridianbettz
felister
sidhani Kama spurs watakubali dier aondoke
Rehema
Ni vizuri
farida ahmadi
Safiiii sana
Hope mwaikuka
Inapendeza
David Pere
Good news 👍👍