Klabu ya Dodoma Jiji imepata ushindi wake wa kwanza wa NBC Primia Ligi toka msimu huu uanze ambapo hii leo akiwa mwenyeji  ameondoka na alama tatu muhimu ambazo amezitafuta katika mechi nne zilizopita na kuzikosa.

 

Dodoma Jiji Yapata Ushindi Wake wa Kwanza

Dodoma Jiji walikuwa wakikipiga na Wachimba Madini Geita Gold ambapo wameshinda kwa ushindi kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika dakika ya 23 kupitia kwa mchezaji wao Collins Opare na ndilo bao pekee lililosalia hadi mpira kumalizika.

Ushindi huo umewapeleka walima zabibu  hadi nafasi ya 9 huku wakiwa na kazi kubwa ya kufanya kwani kadri wanavyozidi kwenda taratibu siku nazo zinakwenda wanaweza shangaa ligi inaisha wapo hatarini.

Wakati kwa upande wa Geita wao wameanza vibaya msimu huu tofauti na zamani kwani wao mpaka sasa hawajashinda mchezo wowote. Klabu hiyo msimu uliopita walifanya vizuri na kumaliza wakiwa nafasi ya nne, kitu ambacho kiliwafanya washiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika lakini wameshatolewa katika hatua za mwanzo.

 

Dodoma Jiji Yapata Ushindi Wake wa Kwanza

Timu hiyo ambayo kocha wake mkuu ni Fred Felix Minziro ilipanda daraja msimu uliopita na ilileta ushindani mkubwa katika ligi huku ikitoa mfungaji bora wa ligi George Mpole akimpiku Fiston Kalala Mayele wa Yanga. Mpaka sasa ana sare tatu na kapoteza mara tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa