Emile Smith Rowe kiungo wa klabu ya Arsenal amefanyiwa upasuaji baada ya kuumia siku baada ya kuumia kwa nyonga yake siku kadhaa nyuma na tarifa imetoka leo kua mchezaji huyo kafanyiwa upasuaji.

emile smith roweKiungo huyo ambaye alikua na msimu mzuri mwaka 2021/22 akiwa kama miongoni mwa wachezaji tegemezi kwenye kikosi cha mwalimu Mikel Arteta amekua akiandmwa na majeraha ya mara kwa mara toka msimu huu uanze.

Emile Smith Rowe alikua akisumbuliwa na nyonge zake na kumfanya kushindwa kufanya mazoezi vizuri, Na hapo ndipo timu ya madaktari ya klabu hiyo baada ya mchezo kati yao na Man United na madaktari waliamua mchezaji huyo afanyiwe upasuaji wa nyonga iliyokua inamsumbua.

Mchezaji huyo amekamilisha upasuaji wake vizuri kabisa na timu ya madaktari ya klabu hiyo inaamini mchezaji huyo anaweza kurejea dimba mwezi disemba mwaka huu.

emile smith roweKila mtu kwenye klabu kwasasa atamuunga mkono Emile Smith Rowe ili kuhakikisha anarudi uwanjani haraka iwezekanavyo ili kuendelea kuipambania timu ambayo ni timu ilyomlea kijana huyo toka timu za vijana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa