Cristiano Ronaldo anaweza kuwa zaidi ya mchezaji anayetokea benchi wa Manchester United msimu huu na bado ana mengi ya kutoa, kulingana na golikipa wa zamani wa United enzi za Ferguson Van der Gouw.
Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or ameanza mara moja tu kwenye Primia ligi msimu huu, pia amecheza mechi tano nje ya benchi, na bado hajafunga au kuwa na assist.
Mchezo unaofata utakuwa ni Dabi kati yao na Manchester City siku ya Jumapili, na bado haijafahamika iwapo Meneja Erik ten Hag atamfikiria Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 kuanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye Uwanja wa Etihad.
Mfungaji bora wa msimu uliopita wa mabao 24 kwa United alikosa ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa klabu mwezi Julai kwa sababu za kibinafsi, na ameonekana kukosa makali katika wiki za mwanzo za ushindani.
Raimond van der Gouw, ambaye alikaa United kwa misimu sita wakati wa Alex Ferguson, anahisi kuwa mshambuliaji huyo wa Kireno atakuja vizuri tena, akipendekeza ni suala la kupata wakati sahihi.
Alipoulizwa kama Ronaldo anaweza kuwa mbadala mzuri wa United msimu huu, Van der Gouw aliiambia Stats Perform: “Sitasema hivyo. Hapana, hapana, hapana, hapana”. na kusema kuwa anamaanisha anaweza kufunga mabao zaidi ya 30.
Van der Gouw ambaye ni golikipa wa zamani alisema wiki hizo kabla ya msimu kuanza ni muhimu sana, na mtu yeyote ambaye hayuko kasi wakati hatua ya ushindani inaendelea anaweza kutatizika. Anamwona Ronaldo akitoa zaidi ya wachezaji kutoka benchi siku zijazo na anadhani umri wake bado ni mzuri vya kutosha.
“Unaweza kuwa fiti na kufanya kazi yako kwenye gym, lakini unahitaji usawa wako wa mechi, na unapata hiyo kwa kucheza michezo tu. Na ndivyo hakufanya hapo mwanzo. Kwa hiyo yuko nyuma kidogo.”
Alifunga bao lake la kwanza msimu huu kwenye Ligi ya Europa, kwa penalti dhidi ya Sheriff, kabla ya kwenda kucheza kimataifa. Hata akiwa na Ureno, ambapo alicheza mechi kamili dhidi ya Jamhuri ya Czech na Uhispania, Ronaldo amekuwa bado hayuko sawa.
Baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Uhispania wiki hii kwenye michuano ya ligi ya Mataifa uchezaji wa Ronaldo ulishutumiwa vikali, na kumfanya dada yake, Katia Aveiro kusema kuwasema wakosoaji kuwa ni watu wajinga, wasio na roho na wasio na shukurani.
Ronaldo pia alitetewa na mchezaji mwenzako Bruno Fernandes, ambaye alisema: “Hii ni awamu, mabao yakianza kuonekana atakuwa na uwezo na utulivu zaidi wa kuendelea kuifungia timu yetu ya Taifa. Siwezi kusahau kuwa yeye ndiye mfungaji bora kuwahi kutokea.”
Ronaldo wa miaka iliyopita anaweza kuwajibu wapinzani kwa kutoa matokeo ya ushindi katika mchezo wake unaofuata, lakini benchi inaweza kurejea tena wikendi hii. Van der Gouw hana shaka City itatoa upinzani mkali kwa United.
Van der Gouw alisema kwasasa ni dhahiri City wako mbele zaidi mbele kuliko Man United na hilo liko wazi kabisa, golikipa huyo ambaye kwa miaka mingi alikuwa naibu wa Peter Schmeichel.
“Kila mtu lazima awe mkali sana. Na kisha tutaona nani atakuwa mshindi. Huo ni mchezo mkubwa. Mkubwa.”