Klabu ya Udinese imemuonesha Cristiano Ronaldo mlango wa kuchomokea kutoka Manchester United baada ya Mreno huyo kudai bado hafikirii kustaafu kwa sasa.

christiano Ronaldo
christiano 

Golikipa wa Udinese, Marco Silvestri alijibu post ya Ronaldo kwenye mitandao ya kijamii akimtaka Mreno huyo ajiunge na miamba hiyo ya Italia hali iliyopelekea klabu hiyo kuingilia kati kwa kujibu kwa emojis chini ya maoni (comment) ya Silvestri huku wakihakikisha Mreno huyo anapata maoni yao kwa kum-tag Ronaldo.

Post ya Ronaldo ilisomeka “Matarajio yangu ni makubwa. Nataka kuwepo kwenye Kombe la Dunia na Mashindano ya Euro 2024. Ninajisikia kuhamasika sana. Safari yangu bado haijakamilika.”

Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa tayari kuondoka Manchester United wakati wa usajili wa kiangazi akitaka klabu inayoshiriki ligi ya Mabingwa Ulaya anaweza kushawishiwa na hatua hii ya Udinese ambao wamekuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi kuu Italia wakiwa nafasi ya tatu baada ya kushinda mechi 5 kati ya saba msimu huu.

Hatma ya Ronaldo bado haijulikani licha ya kufunga goli lake la kwanza la msimu mapema mwezi huu. Inaelezwa wachezaji wenzake huko Man United wanaamini ataondoka Januari baada ya kupokea ofa nono kutoka Saudi Arabia.


Kwa habari na matukio ya kimichezo na ya uhakika tembelea Youtube channel yetu Meridian Sport

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa