Kocha wa timu ya taifa ya Wales Rob Page amesema hana wasiwasi na staa wa timu hiyi Gareth Bale alietimkia ligi kuu ya marekani inayofahamika kama Major League Soccer (MLS)katika klabu ya Los Angels Galaxy.

Kocha huyo ameonesha hana hofu na staa wake huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye tangu ajiunge na timu yake hiyo mpya mwezi juni mwaka huu akiwa ameanza michezo miwili pekee huku akiimarisha utimamu wake wa mwili ili kujiandaa na michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Qatar.

kochaWales ambao watashiriki michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka huu toka mwaka 1958 watahitaji kua na wachezaji wao nyota ili kufanya vizuri zaidi.

Bale hakua akicheza michezo mechi kwenye klabu yake ya zamani ya Real Madrid lakini lilipokuja kwenye suala la timu ya Taifa ya Wales aliendelea kucheza kwa kiwango bora kitu kinachomfanya kocha huyo kuamini hata katika kloabu yake kutokupata nafasi sana ya kucheza sio changamoto kwa mchezaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa