Klabu ya Los Angeles FC imethibitisha kumsajiri mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Real Madrid baada ya kumaliza mkataba wake.

Gareth Bale siku ya Jumamosi usiku kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii  alithibitisha anapoelekea kwa kuandika,”Tuoanane hivi karibuni,Los Angeles”.

Gareth Bale

Bale akizungumza kwenye mtandao wa klabu alisema; “Nina furaha kwa uhamisho huu wa kuja Los Angeles Fc, hii ni sehemu sahihi kwangu na familia yangu na ni wakati sahihi kwa kazi yangu, na nina shauku ya kuanza kufanya kazi na niko tayari kushinda makombe zaidi na LAFC.”

Gareth Bale awali alikuwa anahusishwa na timu yake aliyoanzia kucheza soka Cardiff City ambapo walifanya mazungumzo mara kadhaa, pia alishafanya mazungumzo na klabu ya DC united ya  nchini Marekani kabla ya kuamua kwenda LAFC.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa