Mashambuliaji nyota wa kimataifa wa Wales Gareth Bale anaenda kuanza maisha mapya kwenye jiji la California nchini Marekani baada ya kufikia makubaliano na timu ya Los Angeles FC inayoshiriki ligi kuu ya MLS.

Gareth Bale anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na timu, huku kwenye mkataba wake kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba hadi miezi 18, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid anakwenda kukutana na mchezaji nyota aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Juventus Giorgio Chiellini.

Gareth Bale

Gareth Bale alijiunga na Real Madrid akitokea klabu ya Tottenham Hotspur mwaka 2013 na kufanikiwa kushinda mataji matatu ya La Liga, Copa del Rey na mataji matano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 32, pia ameisaidia timu yake ya taifa ya Wales kufuzu michuano ya kombe la dunia, baada ya kukaa miaka 64 pasipo kushiriki michuano hiyo.

Gareth Bale kabla ya kuchugua kuhamia Marerkani kwenye ligi ya MLS, alikuwa na wigo mpana wa kuchagua kwani klabu nyingi zilikuwa zinagombania huduma yake.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa