Klabu ya Bayern Munich imekanusha tetesi za kuwa wanamfuatilia mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo kujiunga na klabu hiyo kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Bayern Munich Hasan Salihamidzic wakati anahojiwa na kituo cha Skysport Ujerumani, ikiwa wako kwenye kinyang’anyiro cha kuwania saini ya mshumbuliaji huyo alinukuliwa akisema.

Ronaldo

“Cristiano ni mchezaji wa daraja la juu, na amekuwa na wakati mzuri kwenye karia yake ya soka. Japokuwa, tetesi zinazunguka sana ni tetesi ambazo hazina ukweli wowote kwenye hilo.”

Cristiano Ronaldo ambaye amerejea kwenye klabu ya Manchester United kwenye dirisha la usajira wa majira ya kiangazi lililopita, baada ya miaka 13 aliyotumika nje ya klabu hiyo.

Ronaldo tokea arejee kwenye klabu ya mashetani wekundu, amefanikiwa kufunga magoli 24, kwenye michezo 38 aliyocheza kwenye mashindano yote msimu ulioisha.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa